Yeremia 6:8
Jeremiah 6:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pokea onyo, ee Yerusalemu, la sivyo nitageukia mbali nawe na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa, asiweze mtu kuishi ndani yake.”
Jeremiah 6:8 in English
Jeremiah 6:8 · Berean Standard Bible
Be forewarned, O Jerusalem, or I will turn away from you; I will make you a desolation, a land without inhabitant.”
Context
6Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:
“Kateni miti mjenge boma
kuzunguka Yerusalemu.
Mji huu ni lazima uadhibiwe,
umejazwa na uonevu. 7Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake,
ndivyo anavyomwaga uovu wake.
Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake,
ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima. 8Pokea onyo, ee Yerusalemu,
la sivyo nitageukia mbali nawe
na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa,
asiweze mtu kuishi ndani yake.” 9Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:
“Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli
kwa uangalifu kama kwenye mzabibu;
pitisha mkono wako kwenye matawi tena,
kama yeye avunaye zabibu.” 10Niseme na nani na kumpa onyo?
Ni nani atakayenisikiliza mimi?
Masikio yao yameziba,*
kwa hiyo hawawezi kusikia.
Neno la Bwana ni chukizo kwao,
hawalifurahii.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.