Yeremia 6:10
Jeremiah 6:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Niseme na nani na kumpa onyo? Ni nani atakayenisikiliza mimi? Masikio yao yameziba,* kwa hiyo hawawezi kusikia. Neno la Bwana ni chukizo kwao, hawalifurahii.
Jeremiah 6:10 in English
Jeremiah 6:10 · Berean Standard Bible
To whom can I give this warning? Who will listen to me? Look, their ears are closed,* so they cannot hear. See, the word of the LORD has become offensive to them; they find no pleasure in it.
Context
8Pokea onyo, ee Yerusalemu,
la sivyo nitageukia mbali nawe
na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa,
asiweze mtu kuishi ndani yake.” 9Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:
“Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli
kwa uangalifu kama kwenye mzabibu;
pitisha mkono wako kwenye matawi tena,
kama yeye avunaye zabibu.” 10Niseme na nani na kumpa onyo?
Ni nani atakayenisikiliza mimi?
Masikio yao yameziba,*
kwa hiyo hawawezi kusikia.
Neno la Bwana ni chukizo kwao,
hawalifurahii. 11Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana,
nami siwezi kuizuia.
“Wamwagie watoto walioko barabarani,
na juu ya vijana waume waliokusanyika;
mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake,
hata nao wazee waliolemewa na miaka. 12Nyumba zao zitapewa watu wengine,
pamoja na mashamba yao na wake zao,
nitakapounyoosha mkono wangu
dhidi ya wale waishio katika nchi,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.