Yeremia 6:12
Jeremiah 6:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nyumba zao zitapewa watu wengine, pamoja na mashamba yao na wake zao, nitakapounyoosha mkono wangu dhidi ya wale waishio katika nchi,” asema Bwana.
Jeremiah 6:12 in English
Jeremiah 6:12 · Berean Standard Bible
Their houses will be turned over to others, their fields and wives as well, for I will stretch out My hand against the inhabitants of the land,” declares the LORD.
Context
10Niseme na nani na kumpa onyo?
Ni nani atakayenisikiliza mimi?
Masikio yao yameziba,*
kwa hiyo hawawezi kusikia.
Neno la Bwana ni chukizo kwao,
hawalifurahii. 11Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana,
nami siwezi kuizuia.
“Wamwagie watoto walioko barabarani,
na juu ya vijana waume waliokusanyika;
mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake,
hata nao wazee waliolemewa na miaka. 12Nyumba zao zitapewa watu wengine,
pamoja na mashamba yao na wake zao,
nitakapounyoosha mkono wangu
dhidi ya wale waishio katika nchi,”
asema Bwana. 13“Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,
wote wana tamaa ya kupata faida zaidi;
manabii na makuhani wanafanana,
wote wanafanya udanganyifu. 14Wanafunga majeraha ya watu wangu
bila uangalifu.
Wanasema, ‘Amani, amani,’
wakati hakuna amani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.