Yeremia 49:33
Jeremiah 49:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Hazori itakuwa makao ya mbweha, mahali pa ukiwa milele. Hakuna yeyote atakayeishi humo; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”
Jeremiah 49:33 in English
Jeremiah 49:33 · Berean Standard Bible
“Hazor will become a haunt for jackals,* a desolation forever. No one will dwell there; no man will abide there.”
Context
31“Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe,
linaloishi kwa kujiamini,”
asema Bwana,
“taifa lisilo na malango wala makomeo;
watu wake huishi peke yao. 32Ngamia wao watakuwa nyara,
nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa.
Wale walio maeneo ya mbali
nitawatawanya pande zote,
nami nitaleta maafa juu yao
kutoka kila upande,”
asema Bwana. 33“Hazori itakuwa makao ya mbweha,
mahali pa ukiwa milele.
Hakuna yeyote atakayeishi humo;
hakuna mtu atakayekaa ndani yake.” 34Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda: 35Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,
ulio tegemeo la nguvu zao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.