Yeremia 49:32
Jeremiah 49:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ngamia wao watakuwa nyara, nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa. Wale walio maeneo ya mbali nitawatawanya pande zote, nami nitaleta maafa juu yao kutoka kila upande,” asema Bwana.
Jeremiah 49:32 in English
Jeremiah 49:32 · Berean Standard Bible
Their camels will become plunder, and their large herds will be spoil. I will scatter to the wind in every direction those who shave their temples; I will bring calamity on them from all sides,” declares the LORD.
Context
30“Kimbieni haraka!
Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,”
asema Bwana.
“Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu;
amebuni hila dhidi yenu. 31“Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe,
linaloishi kwa kujiamini,”
asema Bwana,
“taifa lisilo na malango wala makomeo;
watu wake huishi peke yao. 32Ngamia wao watakuwa nyara,
nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa.
Wale walio maeneo ya mbali
nitawatawanya pande zote,
nami nitaleta maafa juu yao
kutoka kila upande,”
asema Bwana. 33“Hazori itakuwa makao ya mbweha,
mahali pa ukiwa milele.
Hakuna yeyote atakayeishi humo;
hakuna mtu atakayekaa ndani yake.” 34Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.