Yeremia 49:31
Jeremiah 49:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe, linaloishi kwa kujiamini,” asema Bwana, “taifa lisilo na malango wala makomeo; watu wake huishi peke yao.
Jeremiah 49:31 in English
Jeremiah 49:31 · Berean Standard Bible
Rise up, advance against a nation at ease, one that dwells securely,” declares the LORD. “They have no gates or bars; they live alone.
Context
29Hema zao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa;
vibanda vyao vitatwaliwa
pamoja na mali zao zote na ngamia zao.
Watu watawapigia kelele,
‘Hofu kuu iko kila upande!’ 30“Kimbieni haraka!
Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,”
asema Bwana.
“Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu;
amebuni hila dhidi yenu. 31“Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe,
linaloishi kwa kujiamini,”
asema Bwana,
“taifa lisilo na malango wala makomeo;
watu wake huishi peke yao. 32Ngamia wao watakuwa nyara,
nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa.
Wale walio maeneo ya mbali
nitawatawanya pande zote,
nami nitaleta maafa juu yao
kutoka kila upande,”
asema Bwana. 33“Hazori itakuwa makao ya mbweha,
mahali pa ukiwa milele.
Hakuna yeyote atakayeishi humo;
hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.