Yeremia 49:35
Jeremiah 49:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Tazama, nitavunja upinde wa Elamu, ulio tegemeo la nguvu zao.
Jeremiah 49:35 in English
Jeremiah 49:35 · Berean Standard Bible
This is what the LORD of Hosts says: “Behold, I will shatter Elam’s bow, the mainstay of their might.
Context
33“Hazori itakuwa makao ya mbweha,
mahali pa ukiwa milele.
Hakuna yeyote atakayeishi humo;
hakuna mtu atakayekaa ndani yake.” 34Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda: 35Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,
ulio tegemeo la nguvu zao. 36Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamu
toka pande nne za mbingu,
nitawatawanya katika hizo pande nne,
wala hapatakuwa na taifa
ambalo watu wa Elamu waliofukuzwa
hawatakwenda. 37Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao,
mbele yao wale wanaotafuta uhai wao;
nitaleta maafa juu yao,
naam, hasira yangu kali,”
asema Bwana.
“Nitawafuatia kwa upanga
mpaka nitakapowamaliza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.