Yeremia 49:36
Jeremiah 49:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamu toka pande nne za mbingu, nitawatawanya katika hizo pande nne, wala hapatakuwa na taifa ambalo watu wa Elamu waliofukuzwa hawatakwenda.
Jeremiah 49:36 in English
Jeremiah 49:36 · Berean Standard Bible
I will bring the four winds against Elam from the four corners of the heavens, and I will scatter them to all these winds. There will not be a nation to which Elam’s exiles will not go.
Context
34Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda: 35Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,
ulio tegemeo la nguvu zao. 36Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamu
toka pande nne za mbingu,
nitawatawanya katika hizo pande nne,
wala hapatakuwa na taifa
ambalo watu wa Elamu waliofukuzwa
hawatakwenda. 37Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao,
mbele yao wale wanaotafuta uhai wao;
nitaleta maafa juu yao,
naam, hasira yangu kali,”
asema Bwana.
“Nitawafuatia kwa upanga
mpaka nitakapowamaliza. 38Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu
na kumwangamiza mfalme wake na maafisa wake,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.