Yeremia 30:5
Jeremiah 30:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Vilio vya woga vinasikika: hofu kuu, wala si amani.
Jeremiah 30:5 in English
Jeremiah 30:5 · Berean Standard Bible
Yes, this is what the LORD says: “A cry of panic is heard— a cry of terror, not of peace.
Context
3Siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘nitakapowaleta watu wangu Israeli na Yuda kutoka uhamishoni, na kuwarudisha katika nchi niliyowapa baba zao ili kuimiliki,’ asema Bwana.” 4Haya ndiyo maneno Bwana aliyoyanena kuhusu Israeli na Yuda: 5“Hili ndilo asemalo Bwana:
“ ‘Vilio vya woga vinasikika:
hofu kuu, wala si amani. 6Ulizeni na mkaone:
Je, mwanaume aweza kuzaa watoto?
Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu
ameweka mikono yake tumboni
kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa,
kila uso ukigeuka rangi kabisa? 7Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha!
Hakutakuwa na nyingine mfano wake.
Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo,
lakini ataokolewa kutoka hiyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.