Yeremia 30:7
Jeremiah 30:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha! Hakutakuwa na nyingine mfano wake. Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo, lakini ataokolewa kutoka hiyo.
Jeremiah 30:7 in English
Jeremiah 30:7 · Berean Standard Bible
How awful that day will be! None will be like it! It is the time of Jacob’s distress, but he will be saved out of it.
Context
5“Hili ndilo asemalo Bwana:
“ ‘Vilio vya woga vinasikika:
hofu kuu, wala si amani. 6Ulizeni na mkaone:
Je, mwanaume aweza kuzaa watoto?
Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu
ameweka mikono yake tumboni
kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa,
kila uso ukigeuka rangi kabisa? 7Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha!
Hakutakuwa na nyingine mfano wake.
Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo,
lakini ataokolewa kutoka hiyo. 8“ ‘Katika siku ile,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,
‘nitaivunja nira kutoka shingoni mwao
na kuvipasua vifungo vyao;
wageni hawatawafanya tena watumwa. 9Badala yake, watamtumikia Bwana, Mungu wao
na Daudi mfalme wao,
nitakayemwinua kwa ajili yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.