Native Bible

Jeremiah 30:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Haya ndiyo maneno Bwana aliyoyanena kuhusu Israeli na Yuda:

Jeremiah 30:4 in English

Jeremiah 30:4 · Berean Standard Bible

These are the words that the LORD spoke concerning Israel and Judah.

Context

2“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Andika katika kitabu maneno yote niliyonena na wewe. 3Siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘nitakapowaleta watu wangu Israeli na Yuda kutoka uhamishoni, na kuwarudisha katika nchi niliyowapa baba zao ili kuimiliki,’ asema Bwana.” 4Haya ndiyo maneno Bwana aliyoyanena kuhusu Israeli na Yuda: 5“Hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Vilio vya woga vinasikika: hofu kuu, wala si amani. 6Ulizeni na mkaone: Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu ameweka mikono yake tumboni kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa, kila uso ukigeuka rangi kabisa?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.