Yeremia 2:12
Jeremiah 2:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Shangaeni katika hili, ee mbingu, nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” asema Bwana.
Jeremiah 2:12 in English
Jeremiah 2:12 · Berean Standard Bible
Be stunned by this, O heavens; be shocked and utterly appalled,” declares the LORD.
Context
10Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu* nawe uangalie,
tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini,
uone kama kumekuwepo kitu kama hiki. 11Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote?
(Hata ingawa hao si miungu kamwe.)
Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao
kwa sanamu zisizofaa kitu. 12Shangaeni katika hili, ee mbingu,
nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,”
asema Bwana. 13“Watu wangu wametenda dhambi mbili:
Wameniacha mimi,
niliye chemchemi ya maji yaliyo hai,
nao wamejichimbia visima vyao wenyewe,
visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji. 14Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa?
Kwa nini basi amekuwa mateka?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.