Native Bible

Jeremiah 2:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu.

Jeremiah 2:11 in English

Jeremiah 2:11 · Berean Standard Bible

Has a nation ever changed its gods, though they are no gods at all? Yet My people have exchanged their Glory * for useless idols.

Context

9“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema Bwana. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako. 10Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu* nawe uangalie, tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, uone kama kumekuwepo kitu kama hiki. 11Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu. 12Shangaeni katika hili, ee mbingu, nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” asema Bwana. 13“Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.