Yeremia 2:14
Jeremiah 2:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa? Kwa nini basi amekuwa mateka?
Jeremiah 2:14 in English
Jeremiah 2:14 · Berean Standard Bible
Is Israel a slave? Was he born into slavery? Why then has he become prey?
Context
12Shangaeni katika hili, ee mbingu,
nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,”
asema Bwana. 13“Watu wangu wametenda dhambi mbili:
Wameniacha mimi,
niliye chemchemi ya maji yaliyo hai,
nao wamejichimbia visima vyao wenyewe,
visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji. 14Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa?
Kwa nini basi amekuwa mateka? 15Simba wamenguruma;
wamemngurumia.
Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa;
miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu. 16Pia watu wa Memfisi* na Tahpanhesi*
wamevunja taji ya kichwa chako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.