Native Bible

Isaiah 62:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo wanao* watakavyokuoa wewe; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

Isaiah 62:5 in English

Isaiah 62:5 · Berean Standard Bible

For as a young man marries a young woman, so your sons will marry you; and as a bridegroom rejoices over his bride, so your God will rejoice over you.

Context

3Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana, taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba,* nayo nchi yako itaitwa Beula,* kwa maana Bwana atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa. 5Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo wanao* watakavyokuoa wewe; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 6Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu, hawatanyamaza mchana wala usiku. Ninyi wenye kumwita Bwana, msitulie, 7msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu na kuufanya uwe sifa ya dunia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.