Isaya 62:7
Isaiah 62:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu na kuufanya uwe sifa ya dunia.
Isaiah 62:7 in English
Isaiah 62:7 · Berean Standard Bible
nor give Him any rest until He establishes Jerusalem and makes her the praise of the earth.
Context
5Kama vile kijana aoavyo mwanamwali,
ndivyo wanao* watakavyokuoa wewe;
kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake,
ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 6Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu,
hawatanyamaza mchana wala usiku.
Ninyi wenye kumwita Bwana,
msitulie, 7msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu
na kuufanya uwe sifa ya dunia. 8Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume
na kwa mkono wake wenye nguvu:
“Kamwe sitawapa tena adui zenu
nafaka zenu kama chakula chao;
kamwe wageni hawatakunywa tena
divai mpya ambayo mmeitaabikia, 9lakini wale waivunao nafaka wataila
na kumsifu Bwana,
nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake
katika nyua za patakatifu pangu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.