Native Bible

Isaiah 62:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana, taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako.

Isaiah 62:3 in English

Isaiah 62:3 · Berean Standard Bible

You will be a crown of glory in the hand of the LORD, a royal diadem in the palm of your God.

Context

1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko, wokovu wake kama mwanga wa moto. 2Mataifa wataona haki yako, nao wafalme wote wataona utukufu wako; wewe utaitwa kwa jina jipya lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka. 3Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana, taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba,* nayo nchi yako itaitwa Beula,* kwa maana Bwana atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa. 5Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo wanao* watakavyokuoa wewe; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.