Native Bible

Isaiah 62:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mataifa wataona haki yako, nao wafalme wote wataona utukufu wako; wewe utaitwa kwa jina jipya lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka.

Isaiah 62:2 in English

Isaiah 62:2 · Berean Standard Bible

Nations will see your righteousness, and all kings your glory. You will be called by a new name that the mouth of the LORD will bestow.

Context

1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko, wokovu wake kama mwanga wa moto. 2Mataifa wataona haki yako, nao wafalme wote wataona utukufu wako; wewe utaitwa kwa jina jipya lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka. 3Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana, taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba,* nayo nchi yako itaitwa Beula,* kwa maana Bwana atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.