Native Bible

Isaiah 62:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba,* nayo nchi yako itaitwa Beula,* kwa maana Bwana atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa.

Isaiah 62:4 in English

Isaiah 62:4 · Berean Standard Bible

No longer will you be called Forsaken,* nor your land named Desolate;* but you will be called Hephzibah,* and your land Beulah;* for the LORD will take delight in you, and your land will be His bride.

Context

2Mataifa wataona haki yako, nao wafalme wote wataona utukufu wako; wewe utaitwa kwa jina jipya lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka. 3Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana, taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba,* nayo nchi yako itaitwa Beula,* kwa maana Bwana atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa. 5Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo wanao* watakavyokuoa wewe; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 6Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu, hawatanyamaza mchana wala usiku. Ninyi wenye kumwita Bwana, msitulie,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.