Native Bible

Isaiah 33:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Sasa nitainuka,” asema Bwana. “Sasa nitatukuzwa; sasa nitainuliwa juu.

Isaiah 33:10 in English

Isaiah 33:10 · Berean Standard Bible

“Now I will arise,” says the LORD. “Now I will lift Myself up. Now I will be exalted.

Context

8Njia kuu zimeachwa, hakuna wasafiri barabarani. Mkataba umevunjika, mashahidi wake wamedharauliwa,* hakuna yeyote anayeheshimiwa. 9Ardhi inaomboleza* na kuchakaa, Lebanoni imeaibika na kunyauka, Sharoni ni kama Araba, nayo Bashani na Karmeli wanapukutisha majani yao. 10“Sasa nitainuka,” asema Bwana. “Sasa nitatukuzwa; sasa nitainuliwa juu. 11Mlichukua mimba ya makapi, mkazaa mabua, pumzi yenu ni moto uwateketezao. 12Mataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa, kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.