Isaya 19:14
Isaiah 19:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana amewamwagia roho ya kizunguzungu; wanaifanya Misri iyumbayumbe katika yale yote inayoyafanya, kama vile mlevi ayumbayumbavyo katika kutapika kwake.
Isaiah 19:14 in English
Isaiah 19:14 · Berean Standard Bible
The LORD has poured into her a spirit of confusion. Egypt has been led astray in all she does, as a drunkard staggers through his own vomit.
Context
12Wako wapi sasa watu wako wenye hekima?
Wao wakuonyeshe na kukufahamisha
ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote
amepanga dhidi ya Misri. 13Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,
viongozi wa Memfisi* wamedanganyika,
walio mawe ya pembe ya taifa lake
wameipotosha Misri. 14Bwana amewamwagia
roho ya kizunguzungu;
wanaifanya Misri iyumbayumbe
katika yale yote inayoyafanya,
kama vile mlevi ayumbayumbavyo
katika kutapika kwake. 15Misri haiwezi kufanya kitu chochote,
cha kichwa wala cha mkia,
cha tawi la mtende wala cha tete. 16Katika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa Bwana Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.