Isaya 19:15
Isaiah 19:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Misri haiwezi kufanya kitu chochote, cha kichwa wala cha mkia, cha tawi la mtende wala cha tete.
Isaiah 19:15 in English
Isaiah 19:15 · Berean Standard Bible
There is nothing Egypt can do— head or tail, palm or reed.
Context
13Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,
viongozi wa Memfisi* wamedanganyika,
walio mawe ya pembe ya taifa lake
wameipotosha Misri. 14Bwana amewamwagia
roho ya kizunguzungu;
wanaifanya Misri iyumbayumbe
katika yale yote inayoyafanya,
kama vile mlevi ayumbayumbavyo
katika kutapika kwake. 15Misri haiwezi kufanya kitu chochote,
cha kichwa wala cha mkia,
cha tawi la mtende wala cha tete. 16Katika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa Bwana Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao. 17Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho Bwana Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.