Native Bible

Isaiah 19:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu, viongozi wa Memfisi* wamedanganyika, walio mawe ya pembe ya taifa lake wameipotosha Misri.

Isaiah 19:13 in English

Isaiah 19:13 · Berean Standard Bible

The princes of Zoan have become fools; the princes of Memphis * are deceived. The cornerstones of her tribes have led Egypt astray.

Context

11Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”? 12Wako wapi sasa watu wako wenye hekima? Wao wakuonyeshe na kukufahamisha ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote amepanga dhidi ya Misri. 13Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu, viongozi wa Memfisi* wamedanganyika, walio mawe ya pembe ya taifa lake wameipotosha Misri. 14Bwana amewamwagia roho ya kizunguzungu; wanaifanya Misri iyumbayumbe katika yale yote inayoyafanya, kama vile mlevi ayumbayumbavyo katika kutapika kwake. 15Misri haiwezi kufanya kitu chochote, cha kichwa wala cha mkia, cha tawi la mtende wala cha tete.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.