Native Bible

Isaiah 19:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wako wapi sasa watu wako wenye hekima? Wao wakuonyeshe na kukufahamisha ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote amepanga dhidi ya Misri.

Isaiah 19:12 in English

Isaiah 19:12 · Berean Standard Bible

Where are your wise men now? Let them tell you and reveal what the LORD of Hosts has planned against Egypt.

Context

10Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa, nao vibarua wataugua moyoni. 11Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”? 12Wako wapi sasa watu wako wenye hekima? Wao wakuonyeshe na kukufahamisha ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote amepanga dhidi ya Misri. 13Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu, viongozi wa Memfisi* wamedanganyika, walio mawe ya pembe ya taifa lake wameipotosha Misri. 14Bwana amewamwagia roho ya kizunguzungu; wanaifanya Misri iyumbayumbe katika yale yote inayoyafanya, kama vile mlevi ayumbayumbavyo katika kutapika kwake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.