Isaya 19:10
Isaiah 19:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa, nao vibarua wataugua moyoni.
Isaiah 19:10 in English
Isaiah 19:10 · Berean Standard Bible
The workers in cloth * will be dejected, and all the hired workers will be sick at heart.
Context
8Wavuvi watalia na kuomboleza,
wale wote watupao ndoano katika Mto Naili,
watadhoofika kwa majonzi. 9Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa,
wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo. 10Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa,
nao vibarua wataugua moyoni. 11Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa,
washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga.
Unawezaje kumwambia Farao,
“Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima,
mwanafunzi wa wafalme wa zamani”? 12Wako wapi sasa watu wako wenye hekima?
Wao wakuonyeshe na kukufahamisha
ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote
amepanga dhidi ya Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.