Isaya 14:17
Isaiah 14:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa, aliyeipindua miji yake, na ambaye hakuwaachia mateka wake waende nyumbani?”
Isaiah 14:17 in English
Isaiah 14:17 · Berean Standard Bible
who turned the world into a desert and destroyed its cities, who refused to let the captives return to their homes?”
Context
15Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu,
hadi kwenye vina vya shimo. 16Wale wanaokuona wanakukazia macho,
wanatafakari hatima yako:
“Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia
na kufanya falme zitetemeke, 17yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa,
aliyeipindua miji yake,
na ambaye hakuwaachia mateka wake
waende nyumbani?” 18Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima
kila mmoja katika kaburi lake. 19Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako
kama tawi lililokataliwa,
umefunikwa na waliouawa
pamoja na wale waliochomwa kwa upanga,
wale washukao mpaka
kwenye mawe ya shimo.
Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.