Isaya 14:15
Isaiah 14:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu, hadi kwenye vina vya shimo.
Isaiah 14:15 in English
Isaiah 14:15 · Berean Standard Bible
But you will be brought down to Sheol, to the lowest depths of the Pit.
Context
13Ulisema moyoni mwako,
“Nitapanda juu hadi mbinguni,
nitakiinua kiti changu cha enzi
juu ya nyota za Mungu,
nitaketi nimetawazwa
juu ya mlima wa kusanyiko,
kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. 14Nitapaa juu kupita mawingu,
nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.” 15Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu,
hadi kwenye vina vya shimo. 16Wale wanaokuona wanakukazia macho,
wanatafakari hatima yako:
“Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia
na kufanya falme zitetemeke, 17yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa,
aliyeipindua miji yake,
na ambaye hakuwaachia mateka wake
waende nyumbani?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.