Mwanzo 6:9
Genesis 6:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivi ndivyo vizazi vya Noa. Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.
Genesis 6:9 in English
Genesis 6:9 · Berean Standard Bible
This is the account of Noah. Noah was a righteous man, blameless in his generation; Noah walked with God.
Context
7Kwa hiyo Bwana akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” 8Lakini Noa akapata kibali machoni pa Bwana. 9Hivi ndivyo vizazi vya Noa.
Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. 10Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. 11Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.