Native Bible

Genesis 6:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu.

Genesis 6:11 in English

Genesis 6:11 · Berean Standard Bible

Now the earth was corrupt in the sight of God, and full of violence.

Context

9Hivi ndivyo vizazi vya Noa. Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. 10Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. 11Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu. 12Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. 13Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.