Ezekieli 32:7
Ezekiel 32:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu na kuzitia nyota zake giza; nitalifunika jua kwa wingu, nao mwezi hautatoa nuru yake.
Ezekiel 32:7 in English
Ezekiel 32:7 · Berean Standard Bible
When I extinguish you, I will cover the heavens and darken their stars. I will cover the sun with a cloud, and the moon will not give its light.
Context
5Nitatawanya nyama yako juu ya milima
na kujaza mabonde kwa mabaki yako. 6Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka
njia yote hadi milimani,
nayo mabonde yatajazwa na nyama yako. 7Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu
na kuzitia nyota zake giza;
nitalifunika jua kwa wingu,
nao mwezi hautatoa nuru yake. 8Mianga yote itoayo nuru angani
nitaitia giza juu yako;
nitaleta giza juu ya nchi yako,
asema Bwana Mwenyezi. 9Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi
nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,
nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi
ambazo haujapata kuzijua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.