Native Bible

Ezekiel 32:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa, nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi ambazo haujapata kuzijua.

Ezekiel 32:9 in English

Ezekiel 32:9 · Berean Standard Bible

‘I will trouble the hearts of many peoples, when I bring about your destruction among the nations, in countries * you do not know.

Context

7Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu na kuzitia nyota zake giza; nitalifunika jua kwa wingu, nao mwezi hautatoa nuru yake. 8Mianga yote itoayo nuru angani nitaitia giza juu yako; nitaleta giza juu ya nchi yako, asema Bwana Mwenyezi. 9Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa, nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi ambazo haujapata kuzijua. 10Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie, wafalme wao watatetemeka kwa hofu kwa ajili yako nitakapotikisa upanga wangu mbele yao. Siku ya anguko lako kila mmoja wao atatetemeka kila dakika kwa ajili ya maisha yake. 11“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli utakuja dhidi yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.