Ezekieli 32:11
Ezekiel 32:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli utakuja dhidi yako.
Ezekiel 32:11 in English
Ezekiel 32:11 · Berean Standard Bible
For this is what the Lord GOD says: ‘The sword of the king of Babylon will come against you!
Context
9Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi
nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,
nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi
ambazo haujapata kuzijua. 10Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie,
wafalme wao watatetemeka
kwa hofu kwa ajili yako
nitakapotikisa upanga wangu mbele yao.
Siku ya anguko lako
kila mmoja wao atatetemeka
kila dakika kwa ajili ya maisha yake. 11“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli
utakuja dhidi yako. 12Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka
kwa panga za watu mashujaa,
taifa katili kuliko mataifa yote.
Watakivunjavunja kiburi cha Misri,
nayo makundi yake yote
ya wajeuri yatashindwa. 13Nitaangamiza mifugo yake yote
wanaojilisha kando ya maji mengi,
hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu
wala kwato za mnyama
hazitayachafua tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.