Ezekieli 32:5
Ezekiel 32:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitatawanya nyama yako juu ya milima na kujaza mabonde kwa mabaki yako.
Ezekiel 32:5 in English
Ezekiel 32:5 · Berean Standard Bible
I will put your flesh on the mountains and fill the valleys with your remains.*
Context
3“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu
nitautupa wavu wangu juu yako,
nao watakukokota katika wavu wangu. 4Nitakutupa nchi kavu
na kukuvurumisha uwanjani.
Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako
na wanyama wote wa nchi
watajishibisha nyama yako. 5Nitatawanya nyama yako juu ya milima
na kujaza mabonde kwa mabaki yako. 6Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka
njia yote hadi milimani,
nayo mabonde yatajazwa na nyama yako. 7Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu
na kuzitia nyota zake giza;
nitalifunika jua kwa wingu,
nao mwezi hautatoa nuru yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.