Kutoka 25:12
Exodus 25:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine.
Exodus 25:12 in English
Exodus 25:12 · Berean Standard Bible
Cast four gold rings for it and fasten them to its four feet, two rings on one side and two on the other.
Context
10“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,* upana wa dhiraa moja na nusu,* na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 14Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.