Kutoka 25:10
Exodus 25:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,* upana wa dhiraa moja na nusu,* na kimo cha dhiraa moja na nusu.
Exodus 25:10 in English
Exodus 25:10 · Berean Standard Bible
And they are to construct an ark of acacia wood, two and a half cubits long, a cubit and a half wide, and a cubit and a half high.*
Context
8“Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. 9Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha. 10“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,* upana wa dhiraa moja na nusu,* na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.