Native Bible

Exodus 25:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka.

Exodus 25:11 in English

Exodus 25:11 · Berean Standard Bible

Overlay it with pure gold both inside and out, and make a gold molding around it.

Context

9Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha. 10“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,* upana wa dhiraa moja na nusu,* na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.