Native Bible

Exodus 25:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha.

Exodus 25:9 in English

Exodus 25:9 · Berean Standard Bible

You must make the tabernacle and design all its furnishings according to the pattern I show you.

Context

7na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani. 8“Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. 9Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha. 10“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,* upana wa dhiraa moja na nusu,* na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.