Native Bible

Exodus 25:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu.

Exodus 25:13 in English

Exodus 25:13 · Berean Standard Bible

And make poles of acacia wood and overlay them with gold.

Context

11Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 14Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 15Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.