Native Bible

2 Samuel 23:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi: Yosheb-Bashebethi,* Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua katika pambano moja.

2 Samuel 23:8 in English

2 Samuel 23:8 · Berean Standard Bible

These are the names of David’s mighty men: Josheb-basshebeth the Tahchemonite * was chief of the Three.* He wielded his spear against * eight hundred men, whom he killed at one time.

Context

6Lakini watu waovu wote watatupwa kando kama miiba, ambayo haikusanywi kwa mkono. 7Yeyote agusaye miiba hutumia chombo cha chuma au mpini wa mkuki, nayo huchomwa pale ilipo.” 8Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi: Yosheb-Bashebethi,* Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua katika pambano moja. 9Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai,* Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma, 10lakini yeye alisimama imara akawaua Wafilisti hadi mkono wake ukachoka na ukagandamana na upanga. Bwana akawapa ushindi mkubwa siku ile. Vikosi vikarudi kwa Eleazari, kuteka tu nyara za waliokufa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.