2 Samweli 23:9
2 Samuel 23:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai,* Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma,
2 Samuel 23:9 in English
2 Samuel 23:9 · Berean Standard Bible
Next in command was Eleazar son of Dodo * the Ahohite. As one of the three mighty men, he went with David to taunt the Philistines who had gathered for battle at Pas-dammim. The men of Israel retreated,
Context
7Yeyote agusaye miiba
hutumia chombo cha chuma
au mpini wa mkuki,
nayo huchomwa pale ilipo.” 8Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi:
Yosheb-Bashebethi,* Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua katika pambano moja. 9Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai,* Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma, 10lakini yeye alisimama imara akawaua Wafilisti hadi mkono wake ukachoka na ukagandamana na upanga. Bwana akawapa ushindi mkubwa siku ile. Vikosi vikarudi kwa Eleazari, kuteka tu nyara za waliokufa. 11Aliyefuata alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti walipokusanyika pamoja mahali palipokuwa shamba lililojaa dengu, vikosi vya Israeli viliwakimbia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.