1 Samweli 2:6
1 Samuel 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Bwana huua na huleta uhai, hushusha chini mpaka kaburini* na hufufua.
1 Samuel 2:6 in English
1 Samuel 2:6 · Berean Standard Bible
The LORD brings death and gives life; He brings down to Sheol and raises up.
Context
4“Pinde za mashujaa zimevunjika,
lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu. 5Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe
ili kupata chakula,
lakini wale waliokuwa na njaa
hawana njaa tena.
Mwanamke yule aliyekuwa tasa
amezaa watoto saba,
lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi
amedhoofika. 6“Bwana huua na huleta uhai,
hushusha chini mpaka kaburini* na hufufua. 7Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha,
hushusha na hukweza. 8Humwinua maskini kutoka mavumbini
na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu;
huwaketisha pamoja na wakuu
na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha heshima.
“Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya Bwana;
juu yake ameuweka ulimwengu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.