1 Samweli 2:4
1 Samuel 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Pinde za mashujaa zimevunjika, lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu.
1 Samuel 2:4 in English
1 Samuel 2:4 · Berean Standard Bible
The bows of the mighty are broken, but the feeble are equipped with strength.
Context
2“Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Bwana,
hakuna mwingine zaidi yako;
hakuna Mwamba kama Mungu wetu. 3“Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo
wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi,
kwa kuwa Bwana ndiye Mungu ajuaye,
na kwa yeye matendo hupimwa. 4“Pinde za mashujaa zimevunjika,
lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu. 5Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe
ili kupata chakula,
lakini wale waliokuwa na njaa
hawana njaa tena.
Mwanamke yule aliyekuwa tasa
amezaa watoto saba,
lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi
amedhoofika. 6“Bwana huua na huleta uhai,
hushusha chini mpaka kaburini* na hufufua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.