Native Bible

1 Samuel 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi amedhoofika.

1 Samuel 2:5 in English

1 Samuel 2:5 · Berean Standard Bible

The well-fed hire themselves out for food, but the starving hunger no more. The barren woman gives birth to seven, but she who has many sons pines away.

Context

3“Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi, kwa kuwa Bwana ndiye Mungu ajuaye, na kwa yeye matendo hupimwa. 4“Pinde za mashujaa zimevunjika, lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu. 5Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi amedhoofika. 6“Bwana huua na huleta uhai, hushusha chini mpaka kaburini* na hufufua. 7Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.