Wimbo 4:7
Song of Songs 4:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu, hakuna hitilafu ndani yako.
Song of Songs 4:7 in English
Song of Songs 4:7 · Berean Standard Bible
You are altogether beautiful, my darling; in you there is no flaw.
Context
5Matiti yako mawili ni kama wana-paa wawili,
kama wana-paa mapacha
wajilishao katikati ya yungiyungi. 6Hata kupambazuke na vivuli vikimbie,
nitakwenda kwenye mlima wa manemane
na kwenye kilima cha uvumba. 7Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu,
hakuna hitilafu ndani yako. 8Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu,
enda nami kutoka Lebanoni.
Shuka kutoka ncha ya Amana,
kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni,
kutoka mapango ya simba
na kutoka mlima wapendapo kukaa chui. 9Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu;
umeiba moyo wangu
kwa mtazamo mmoja wa macho yako,
kwa kito kimoja cha mkufu wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.