Native Bible

Song of Songs 2:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tazama! Wakati wa masika umepita, mvua imekwisha na ikapita.

Song of Songs 2:11 in English

Song of Songs 2:11 · Berean Standard Bible

For now the winter is past; the rain is over and gone.

Context

9Mpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana. Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu, akitazama kupitia madirishani, akichungulia kimiani. 10Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, “Inuka, mpenzi wangu, mrembo wangu, tufuatane. 11Tazama! Wakati wa masika umepita, mvua imekwisha na ikapita. 12Maua yanatokea juu ya nchi; majira ya kuimba yamewadia, sauti za njiwa zinasikika katika nchi yetu. 13Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni, zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri. Inuka, njoo mpenzi wangu. Mrembo wangu, tufuatane.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.