Wimbo 2:10
Song of Songs 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, “Inuka, mpenzi wangu, mrembo wangu, tufuatane.
Song of Songs 2:10 in English
Song of Songs 2:10 · Berean Standard Bible
My beloved calls to me, “Arise, my darling. Come away with me, my beautiful one.
Context
8Sikiliza! Mpenzi wangu!
Tazama! Huyu hapa anakuja,
akirukaruka juu milimani
akizunguka juu ya vilima. 9Mpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana.
Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu,
akitazama kupitia madirishani,
akichungulia kimiani. 10Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia,
“Inuka, mpenzi wangu,
mrembo wangu, tufuatane. 11Tazama! Wakati wa masika umepita,
mvua imekwisha na ikapita. 12Maua yanatokea juu ya nchi;
majira ya kuimba yamewadia,
sauti za njiwa zinasikika
katika nchi yetu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.