Zaburi 84:4
Psalms 84:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.
Psalms 84:4 in English
Psalms 84:4 · Berean Standard Bible
How blessed are those who dwell in Your house! They are ever praising You. Selah
Context
2Nafsi yangu inatamani sana,
naam, hata kuona shauku,
kwa ajili ya nyua za Bwana;
moyo wangu na mwili wangu
vinamlilia Mungu Aliye Hai. 3Hata shomoro amejipatia makao,
mbayuwayu amejipatia kiota
mahali awezapo kuweka makinda yake:
mahali karibu na madhabahu yako,
Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mfalme wangu na Mungu wangu. 4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,
wanaokusifu wewe daima. 5Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,
na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. 6Wanapopita katika Bonde la Baka,*
hulifanya mahali pa chemchemi,
pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.