Zaburi 84:5
Psalms 84:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
Psalms 84:5 in English
Psalms 84:5 · Berean Standard Bible
Blessed are those whose strength is in You, whose hearts are set on pilgrimage.
Context
3Hata shomoro amejipatia makao,
mbayuwayu amejipatia kiota
mahali awezapo kuweka makinda yake:
mahali karibu na madhabahu yako,
Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mfalme wangu na Mungu wangu. 4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,
wanaokusifu wewe daima. 5Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,
na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. 6Wanapopita katika Bonde la Baka,*
hulifanya mahali pa chemchemi,
pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.* 7Huendelea toka nguvu hadi nguvu,
hadi kila mmoja afikapo
mbele za Mungu huko Sayuni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.