Native Bible

Psalms 78:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.

Psalms 78:4 in English

Psalms 78:4 · Berean Standard Bible

We will not hide them from their children, but will declare to the next generation the praises of the LORD and His might, and the wonders He has performed.

Context

2Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: 3yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia. 4Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. 5Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao, 6ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.