Zaburi 78:3
Psalms 78:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia.
Psalms 78:3 in English
Psalms 78:3 · Berean Standard Bible
that we have heard and known and our fathers have relayed to us.
Context
1Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu,
sikilizeni maneno ya kinywa changu. 2Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo,
nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: 3yale ambayo tuliyasikia na kuyajua,
yale ambayo baba zetu walituambia. 4Hatutayaficha kwa watoto wao;
tutakiambia kizazi kijacho
matendo yastahiliyo sifa ya Bwana,
uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. 5Aliagiza amri kwa Yakobo
na akaweka sheria katika Israeli,
ambazo aliwaamuru baba zetu
wawafundishe watoto wao,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.